Thursday, May 6, 2010

Maurinho aipa Inter kombe la kwanza




Alikuwa ni Diego Milito aliyewanyamazisha mashabiki wa AS Roma katika dimba la Olimpico na akiwainua mashabiki wa milan waliokuwa wachache uwanjani lakini wengi katika jiji la Milan kushangilia kombe lao la kwanza msimu huu huku wakiyasubiria mengine mawili.

Aliyekuwa na furaha zaidi ni Jose Maurinho ambaye baada ya kuifunga Roma goli moja kwa bila katika mchezo huo wa kombe la ligi la italia, amesema hatimaye ndoto yao ya kwanza imetimia

Inter hivi sasa inapigana kuchukua kombe la ligi kuu ya nchi hiyo pamoja na ligi ya mabingwa barani ulaya.

Ribery kukaa kwa mashabiki fainali ya UEFA


Rufaa ya klabu ya Bayern Munich ya kutaka kupunguziwa kwa adhabu kwa kiungo wake mchezeshaji Frank Ribery imetupiliwa mbali na shirikisho la mpira wa miguu.


Licha ya kutupiliwa mbali rufaa hiyo ya Riery, mwenyekiti wa klabu ya bayern munich, Karl-Heinz Ruminege amesema bado timu yake itaendelea kukata rufaaa hadi waone haki imetendeka kwa kiungo huyo aliyepewa kadi nyekundu katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Lyon.

Wednesday, May 5, 2010

Mourinho: Nipeni heshima yangu


Kocha mkuu wa InterMilan Jose Maurinho amewataka mashabiki wa InterMilan kumpa heshima yake kutokana na kuisaidia klabu hiyo kufika katika fainali ya mabingwa barani ulaya, kombe la italia na sasa timu hiyo inafukuzia taji la ubingwa wa ligi la nchi hiyo.

Kocha huyo raia wa ureno anaamini timu yake ina nafasi ya kubebwa kikombe cha italia hii leo wakati timu yake itakapokuwa ikivaana na AS Roma katika dimba la olimpico.

akiuzungumzia kikosi chake kabla ya mchezo huo, maurinho anasikitishwa kwa kumkosa kiungo wake mahiri Sjneider pamoja na mlinzi wake mahiri kutoka brazil Lucio lakini bado anaamini atafanya vizuri katika mchezo huo.

Alipoulizwa kuhusiana na nini anachokikumbuka tarehe tano ya mwezi wa tano, kocha hyo mwenye visanga vingi amesema anachokumbuka ni kifo cha Napoleone Bonapatre.

Redknapp: Pressure ipo kwa Man city sio sisi




Kocha mkuu wa klabu ya totenham hotspurs, harry redknapp amesema presha kwa sasa ipo kwa man city na sio kwa klabu yake,.

redknapp moja ya makocha wanaoheshimika sana nchini uingereza ametoa kauli hiyo kabla ya miamba hiyo miwili kuvaana usiku wa leo katika mchezo unaoweza ukaamua ni nani atamaliza katika nafasi ya nne na hatimaye kushiriki katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya.

Kocha huyo wa zamani wa klabu ya portsmouth amesema kuwa wakati ligi inaanza watu wengi waliipigia chapuo man city kumaliza ya nne hivyo anaamini wapinzani wao watashuka dimbani kwa kupania ili watmize adhma yao lakini huku wakihofi timu yake kushinda kwani kama ikishinda leo itakuwa imejihakikishia kabisa kucheza ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao.

Wednesday, March 3, 2010

Brazil yaichapa Ireland 2-0 uwanja wa emirates, London


Robinho akishangilia goli la pili aliofunga kiufundi na kumzidi maarifa mmoja kati ya makipa bora duniani Shy Given

Tuesday, March 2, 2010

Capello awaonya wachezaji wake


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya uingereza fabio capello amewataka wachezaji wake kusahau matatizo yao binafi yanayowakabili na badala yake waelekeze nguvu zao katika kujiandaa na fainali za dunia.

John Terry na Wayne Bridge wamekuwa katika ugomvi mkubwa wa mapenzi hai iliyomfanya Bridge kujiondoa katika kikosi cha timu ya taifa cha nchi hiyo huku Ashley Cole akiwa ana matatizo na mkewe abaada ya kusaliti ndoa yao

Uingereza inacheza na misri usiku wa leo ktika mchezo wa kujipima nguvu